Kutoka kushoto ni bidada Eshe akiwa amembeba mtoto Yasmeen na anayefuata ni mama mzazi wa Yasmeen bidada Warda na wa mwisho ni mama Ahmed,ni jana kwenye maulid ya mtoto Yasmeen.
Mzaa chema mama Yasmeen akiwa  amekumbati zawadi nyingi za mtoto wake kipenzi hapo jana.
Mash`Allah mtoto Yasmeen aliwa amepozi akipokea dua alizokuwa akiombewa na wanandugu,jamaa na marafiki waliofika kwenye maulid hiyo hapo jana.
Bidada Zuhra ambaye alihudhuria maulid ya mtoto Yasmeen,na wengineo wanaonekana ni mabibi walifika kwenye maulid ya mjukuu wao.
Pichani kushoto mama Leyla na bidada Anita ambao walikuwepo kwenye maulid hiyo jana.
Pichani kulia ni bidada Ramla ambaye ni shangazi wa mtoto Yasmeen na kulia kwa bidada Ramla ni mama Sophy ama mrs J.
 Kushoto ni mama Naima na shoga yake kipenzi walikuwepo kwenye shughuli ya maulid hapo jana.
Kutoka kushoto ni Mrs Aziz na mtoto wake Junior,bidada Hadija na mama Leyla wakipata kumbukumbu ya maulid hapo jana.
Mrs Jimmy(Betty) kushoto na shoga yake  nae anajulikana kwa jina la Betty.
Mama Leyla,Hadija,bidada Saada Baraka na mrs Jimmy ama Betty wakipata flash kuweka mambo sawa kwenye kumbukumbu.
Kuhusu madikodiko na mapochopocho kwa kweli walifaidi wakina mama peke yao,maulidi hii iliyofana vizuri ilihudhuriwa na kina mama peke yao na hakukuwa na mwanaume hata mmoja.Maganga One blog inamtakia kila la heri mtoto Yasmeen kwenye makuzi na malezi yaliyo bora na misingi ya dini ya wazazi wake(Islam). (picha na mama leyla wa Maganga One Blog).