Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Hamza Mnadi (27), mkazi wa Mtaa wa Kalanje Wilaya ya Tunduru kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya cocaine na heroine.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema tukio hilo lilitokea Aprili 7, mwaka huu saa 11:00 jioni katika mtaa wa Kalanje mjini Tunduru
Alifafanua kuwa dawa hizo zilihifadhiwa katika pakiti tisa ambapo kila pakiti kulikuwa na vipande 25 na kufanya jumla ya vipande 225.
Alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na upelelezi unaendelea.
0 Comments