Usiku wa kuamkia leo nchini Holland huwa hapatoshi kwa pilikapilika za watu kununua bidhaa kwa bei ya kutupa na burudani kila kona.
Siku hii haichagui rika,kabila wala mataifa ni kila mmoja anajumuika uwanjani kununua,kuangali kile kinachompendezea kwa siku hii,ni siku ambayo malkia wa Holland hupendelea kujumuisha jamii kwa kuiita siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama yake mzazi Konningen dag.
Sio tu kununua bidhaa hata michezo ya watoto pia inakuwepo kwa usiku mzima mpaka leo hii.
Kama unavyojionea unaweza kuibahatisha computer nzuri kwa bei ya madafu yani ulaya mambo mswano
Kila kitu kipo yani ni pesa yako tu ndugu yangu.
Live band huwa zinatumbuiza na kila mtu anainjoy burudani mahala hapo
Na kama ni mpenzi wa kumbembea aaaah hapo utabembea mpaka ubembee
Kubembea sio tu lazima wabembee watoto,hata watu wazima kumbea ni afya nzuri kabisaa,kwa mbali anaonekana mama Leyla akijikumbusha enzi zake za kubembea kidongochekundu.
Unaweza kujinyakulia zawadi za watoto,vifaa vya computer na vifaa vya matumizi ya jikoni kwa bei cheeee kabisaa.
Hapo unaweza kumuona Shekh Hija na binti yake Leyla wakipata flash kwenye viwanja vya sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama yake na malkia wa Holland.walipita kwenye madikodiko ya kuvunja mifupa BURGER KING maana kofia haziongopi.(picha na shekh Hija wa Maganga One Blog -Holland).