Kumetokea mlipuko katika Jumba la Tamthilia lililofunguliwa upya katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Mlipuko huo umefanyika wakati wa hafla ya kuamdhimisha mwaka mmoja tangu televisheni ya taifa kuanza kuyapeperusha matangazo yake.
Takriban watu saba wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, wakiwemo wabunge. Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali alikuwepo kwenye hafla hiyo lakini haijabainika ikiwa alijeruhiwa.
Mshambuliaji wa kike wa kujitoa mhanga ameripotiwa kufanya shambulio hilo.
Kundi la Al Shabaab limekuwa likitumia mashambulio ya mhanga kama mbinu mpya ya harakati zake tangu kutimuliwa mjini Mogadishu mwaka jana.