Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akishangilia bao la tatu aliloifungia timu yake. Kulia ni Patrick Mafisango.
Waziri Mkuu mstaafu, Mh Frederick Sumaye akipokea zawadi ya jezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage baada ya kumalizika kwa mchezo. Picha zote na Francis Dande
Timu ya soka ya Simba jioni hii imeifunga bao 3-0 klabu ya Al Ahly Shandy kutoka Sudan katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wekundu wa Msimbazi ndio timu pekee kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyobaki katika michuano yote ya kimataifa inayosimamiwa na CAF, ambapo pia ni wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa.
Simba imejiwekea mazingira mazuri ya kuingia kwenye hatua ya Nane Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kuifunga Al Ahly Shandy mabao 3-0 jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Simba sasa inahitaji sare yoyote kwenye mchezo wa marudiano, au kufungwa si chini ya mabao 2-0 ili kuingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Timu nane zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa zitaungana na timu nane zitakazofozu katika hatua hii ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, kuchuana kuwania nafasi nane za kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
0 Comments