Moja ya vitu ambavyo kwetu ni kinyume ni pale unapoona watu watu wanashangaa mbuzi,ngo`mbe,kuku, kondoo n.k yaani wamewekewa sehemu maalumu ya kushangaa wanyama hao,pichani kama unavyoona mtoto akimpa mbuzi majani na pembeni mwa mtoto huyo kuna watu wengine wanalisha wanyama hao.
Watoto wakiwa wanaogopa kumshika ngo`mbe,wanajaribu kumgusa kwa mbalimbali ili waone kama hawezi kuwang`ata ama vipi...
Hapo kajaribu kumgusa na kuona kwamba hana madhara yoyote
Na mwenziwe akaona isiwe tabu na yeye akaungana na mwenzake kumshika vizuri ngo`mbe huyo
Aisee hapo nilichoka kukutana na bongeeee la kuku nikajiuliza hili Jogoo ama Tee jibu nikalipata nilipopiga hiyo picha ya chini.
Duniani wawili wawili
0 Comments