BARAZA la Wawakilishi limeelezwa kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inashirikishwa kikamilifu katika vikao mbalimbali vya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), pamoja na Ushirikiano wa kikanda.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae, Mohamed Said Mohamed (CCM), aliyetaka kufahamu Zanzibar inashirikishwa vipi katika vikao vya EAC.

Akifafanua zaidi, Dk. Mwinyihaji alisema Zanzibar inashirikishwa katika vikao mbalimbali vinavyofanywa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ikiwemo ya ngazi za wakurugenzi, makatibu wakuu pamoja na mawaziri na hata za viongozi wa ngazi za juu ambavyo ni marais.  Mwinyihaji. Hata hivyo, Dk. Mwinyihaji alisema Zanzibar haiwezi kuwa mwanachama kamili wa EAC kwa mujibu wa Katiba ambapo mambo ya ushirikiano wa kimataifa na kikanda ni masuala ya Muungano.

Alisema kwa mujibu wa makubaliano, Zanzibar inaingia katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kutumia mgongo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kufaidika na mambo mbalimbali.

Aidha, alisema tayari ipo baadhi ya miradi mbalimbali inatarajiwa kutekelezwa na Zanzibar kufaidika ambayo inatoka katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Miradi hiyo itakapoanza kutekelezwa itasaidia kuimarisha huduma za jamii na uchumi na kupunguza umasikini.


“Tunashirikishwa katika vikao vyote vya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuanzia ngazi za wakurugenzi, makatibu wakuu na mawaziri, lakini hata katika vikao vya ngazi za juu Rais wa Zanzibar huwa anaalikwa,” alisema Dk.