Kwa mara ya nyingine tena  jijini Den Haag ni usiku wa burudani kwa wapenzi wa muziki wa Taarabu (rosha roho)
Isha akiwa na tuzo yake hivi karibuni.
Mwanadada mwenye mvuto na sauti ya pekee ISHA MASHAUZI tarehe 15/6/2012 anatarajiwa kufanya show kabambe nchini Holland.akithibitisha ujio wa kuja kwa msanii huyo ambaye ni mdhamini wa show hiyo KING JAMES amezungumza moja kwa moja na Maganga One Blog na kuhakikisha kwamba Isha Mashauzi anakuja kufanya show jijini Den Haag.Hivyo wapenzi wa muziki wa kidole juu mnaombwa kufika kwa wingi na kumpa sapoti mwanadada Isha katika Show hiyo.

Maganga One Blog katika kuliweka hilo sawa ipo mbioni kufanya mawasiliano na Isha mwenyewe ili mumsikie kwa sauti yake kuhusu ujio huo hapa Ulaya.haya wapenzi wa vidole juu kaeni mkao wa kula kujimwayamwaya na Isha Mashauzi.