Nyota wa kike anayetamba ndani ya Bongo Movies, Jacqueline Wolper ameweka wazi ya kuwa dini ya Kiislam ameipenda siku nyingi kabla hajakutana na mpenzi wake Dallas.

Wolper alizungumza hayo kupitia kwenye TV ya Channel Five pale alipoulizwa kama alibadili dini kwa sababu ya mpenzi wake huyo wa sasa. Lakini mrembo huyo alipinga suala hilo na kusema alikuwa akiuupenda uislamu kabla hata hajakutana na Dallas.
“Nakumbuka nilikuwa nikiupenda Uislam na kuweka picha zenye viashiria vya dini hiyo ndani kwangu hivyo Dallas alinikuta tayari ninapenda ndipo nikabadili,”
alisema Wolper.