Kwa wale waliowahi kufika mji wa Leuven jengo kama hili  watakuwa wanalifahamu na kutokea kwenye jengo hili ni umbali wa dk 5 kwa kutembea na miguu mpaka kuufikia ukumbi huo.
Ukifika ukumbini hapo utakutana na jina la ukumbi huo pale mlangoni na jina la ukumbi huo linasomeka kama linavyoonekana hapo juu.
Kwa ndani jinsi ukumbi unavyoonekana unapoingia.
Kwa upande mwingine unaonekana kama hivii 
Kwa wale wapenda mchezo wa poll mambo yatakuwa kama hivii na kuna mchezo wa Darts kwa wapenda Darts na mengine meengi tu mtayakuta humohumo ukumbini.
Yani ni full kujiachia ukumbini humo,maana kwa watakaocheza watacheza,watakao kaa kwenye viti watakaa.

Na huyu ndiye Dj Chill ambaye siku hiyo atatoa burudani ya kipekee...Dj huyu ni Dj mzoefu sana katika shughuli yake hii,na siku hiyo ndiyo uje ujionee mwenyewe jinsi gani atakuonyesha uzoefu wake.

Mratibu wa shughuli hii ndugu Ally Khamis amethibitisha kwa kauli yake kuwa kila kitu kipo sawasawa ni kuisubiri tu siku hiyo ya shughuli.