Warembo 10 wanaowania kuchukua taji la Miss Singida 2012 wakiwa kwenye picha ya pamoja.
                                                                   Zainabu Motie.
                                                                       Rukia Azipa.
                                                                           Elizabeth Simon.
                                                               Esther Samngu.
                                                                  Aisha Khamis.
                                                                   Elizabeth Diamond.
                                                                     Loverness Munissi.
                                                                 Lucrencia Marco.
                                                                  Rehema Marwa.
Picha ya pamoja.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Jumla ya warembo 10,wanashiriki mazoezi makali kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki shindano la kumsaka Miss Singida 2012,linalotarajiwa kufanyika juni mosi mwaka huu, kwenye ukumbi wa Aqua resort vitae,mjini Singida
Warembo hao wanaoshiriki mazoezi hayo ambayo yako chini ya usimamizi wa mratibu wa Miss Redds mkoa wa Singida Aunt Borah Lemmy, warembo hao ni Zainabu Motie na Rukia Azipa, Elizabeth Simon,Esther Samngu,Margereth Peter, Aisha Khamisi,Elizabeth Diamond, Loverness Munissi, Lucrencia Marco na Rehema Marwa.
Akizungumza na MO BLOG, Aunt Borah alisema mazoezi yanaendelea vizuri kama yalivyopangwa
“Kwa kweli warembo wa mwaka huu,wanawajibika kikamilifu katika kufanya mazoezi na wanafuata kwa makini yote tunayowaelekeza kufanya.Hii inanipa picha kwamba shindano la mwaka huu,litakuwa na mchuano mkali sana”,alisema.
Kuhusu zawadi za mwaka huu, Aunt Borah alisema mshindi wa kwanza,atazawadiwa shilingi 400,000/=,wa pili 300,000/= na watatu,ataambulia shilingi 200,000/=.
Alisema mshindi wa nne na tano,kila moja atazawadiwa shilingi laki moja nma nusu na washiriki wengine waliosalia,watapewa shilingi laki moja kwa ushiriki wao.
Wakati huo huo,mratibu huyo alisema kuwa msanii maarufu wa taarabu nchini,Khadija Kopa,anatarajiwa kuingia mjini Sindida jioni ya leo (31/5/2012).