Uturuki imewatoa maafisa wote wa kibalozi kutoka Syria siku tatu kuondoka nchini humo.
Hatua sawa na hiyo imechukuliwa na Japan ambayo imemfukuza balozi wa Syria kutoka Tokyo.
Hatua ya sasa inafuatia lawama za kimataifa kufuatia mauaji ya halaiki Ijumaa iliyopita katika eneo la Houla.
Kundi la wapiganaji watiifu kwa serikali limelaumiwa kwa mauaji ya wanawake na watoto.
Syria nayo imemfukuza balozi wa Uholanzi ambaye alikuwa amesalia mjini Damascus kutoka Magharibi.
Shirika la habari la taifa nchini Syria limelaumu nchi za Magharibi kwa kuchochea uhasama zaidi na kuhujumu mpango wa amani.