Mtu aliyekuwa na bunduki amemuuwa mpatanishi mkuu wa amani nchini Afghanistan Arsala Rahmani.
Zamani Bwana Rahmani alikuwa afisa wa Taliban lakini baadae akawa kati ya watu wa mwanzo kujiunga na juhudi za kutafuta amani.

Polisi wanasema alipigwa risasi akiwa anaendesha gari kuelekea kazini.

Afisa mwandamizi wa Rais Hamid Karzai, alikiambia Chanzo  kwamba Bwana Rahmani alikuwa mjumbe muhimu katika baraza la amani la Afghanistan, lilobuniwa miaka miwili iliyopita kuanzisha mazungumzo na Taliban.

Afisa huyo amesema Rais Karzai alikuwa akimtegemea sana kwa ushauri wake, kwa kuwa alielewa vema mawazo ya Taliban.

Mauji ya Bwana Rahman yanafuatia yale ya mwenyekiti wa baraza la amani, Burhanuddin Rabbani mwezi wa Septemba.