Pichani mabondia wawili ambao wamekuwa wakitambiana kuwa kila mmoja hamuhofia mwenzake wakiwa katika kipindi cha maswali na majibu kwa waandishi wa habari siku za nyuma.waandaji wa siku hiyo walidiriki kuweka kizuizi ili kuepuka mtafaruku kati ya wababe hao. 
Pichani kulia mwenye kofia ni bondia Chisora na upande wa kushoto aliyesuka nywele ni bondia Haye.Kiukweli mpambano huu unasubiriwa kwa hamu kubwa sana kutokana na kila mmoja wao kujigamba sana kwamba ana uwezo zaidi ya mwenzake.Pambano litafanyika siku ya jumamosi july 14 mwaka huu 2012.