Huku ulimwengi ikiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari, mwandishi mmoja wa habari wa kituo cha redio cha Daljir, nchini Somalia, ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu walio kuwa wamejihami kwa silaha kali mjini Galkayo Kaskazini mwa nchi.

Hilo ni tukio la tano la mauaji ya aina hiyo kufanyika mwaka huu.

Mwandishi wenzake wa habari wa kituo hicho cha redio, Farhan Jeemis Abdulle, amesema kuwa wakati akitoka ofisini, walifyatuliwa risasi na watu walikuwa wameficha nyuso zao.

Shirika la Uhuru wa Vyombo vya Habari la Reporters Without Borders, limesema Somalia ni nchi hatari kuliko zote kwa mtu kufanyakazi ya uandishi wa habari.

Zaidi ya waandishi wa habari 30 wameuawa katika kipindi cha miaka 5 iliyopita Somalia