Zaidi ya nusu ya raia wa Sudan Kusini wanakabiliwa na baa la njaa.
Shirika la chakula duniani limesema kuwa hali hiyo imechangiwa pakubwa na machafuko kati ya Sudan Kusini na jirani zao Sudan.

Shirika hilo limesema kuwa mapigano katika maeneo ya mipaka na pia kufungwa kwa visima kadhaa vya mafuta kumetatiza uchumi wa Sudan Kusini.

Ripoti hiyo inaonya kuwa kadiri machafuko yanavyoendelea kati ya Sudan na Sudan Kusini ndivyo baa la njaa linazidi kutatiza wa Sudan Kusini.

Hapa awali ilikadiriwa kuwa watu takriban milioni 4.7 walikuwa wanakabiliwa na njaa. Lakini sasa yaonekana hali ni mbaya zaidi.
Nchi hiyo kwa wakati huu inahitaji nafaka tani nusu milioni.

Barabara mbovu zinafanya mambo kuwa magumu zaidi kwani usambazaji wa vyakula huwa vigumu zaidi.