Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, anapambana vikali kuhifadhi wadhifa huo baada ya mjadala kuhusu uchaguzi katika televisheni kufanyika leo ambapo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema alishindwa kumbwaga mpinzani wake.
Huku uchaguzi wa duru ya pili ukitarajiwa kufanyika Jumapili, mjadala huo ulionekana kuwa nafasi ya pekee ya Bwana Sarkozy, kurekebisha nakisi ya kura alizopata katika duru ya kwanza ya uchaguzi.
Matokeo ya kura ya maoni yamebainisha kuwa Sarkozy yuko nyuma ya mpinzani wake kutoka chama cha Kisoshalisti Bwana Francois Hollande kwa pointi sita.
Wakati Bwana Sarkozy akimshambulia mpinzani wake katika mjadala Bwana Hollande kwa kumshutumu kuwa uwongo, Bwana Hollande alitulia na kusema rais Sarkozy anakataa kuwajibika kwa rekodi yake ya uongozi.