Kuna mdau toka wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro(jina tunalo)  ambaye ameleta malalamiko yake kupitia Maganga One Blog kwamba-
                               ``Serikali ituangalie na sisi wa vijijini kwa sababu tunajua kwamba rais wa awamu ya tatu alifuta ada za shule za msingi na mtihani wa darasa la nne na la saba ukawa bure,lakini huku kwetu tunalipia,sasa sisi sijui ni nchi gani,darasa la nne michango yote jumla ni (24,000/= kwa mwaka) na darasa la saba (65,000/=kwa mwaka) je sisi sio watanzania kama vijiji vingine?``

Mwisho.
Pole kwa kazi Mr Maganga na asante kwa kuzirusha habari zetu.