Viazi,Muhogo,Karanga,Asali na Maziwa ndivyo vimenikuza mimi jamani...hata niende wapi hata niishi na watu wa aina gani huwa sifichi asilia yangu kuwa hivi ndivyo vimenikuza mimi na mpaka leo naoneka mtu mwenye afya nzuri.napenda sana chakula hiki jamani. 
Unaweza kuweka chipsi kuku au chipsi mayai ila mimi nitachagua viazi kwa mihogo ya kuchemsha kwa karanga na asali pembeni aaah mie hapo mpaka navimbiwa.Waungwana nawatakia sikukuu njema kwa kila mmoja wetu na wapenzi wote wa Maganga One Blog kwa kushirikiana vyema kuendeleza blog yetu.leo nami nimeona nichukue fursa hii kupumzika na familia kwa kunyoosha miguu hapa na pale,tukutane tena kesho kwenye kurasa zetu kama kawaida.Ahsanteni sana nategemea nitakuwa nimeeleweka.