Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda(kulia) akimkabidhi Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Captain Erenest Mwanossa (kushoto) mwenge wa Uhuru leo mjini Mbeya tayari kwa kuanza mbio kwa ajili ya mwaka 2012.
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dr. Fennella Mukangara (kushoto) akimtambulisha Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge,Captain Erenest Mwanossa kwa Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2012 zilizofanyika leo jijini Mbeya.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (kushoto) wakibadilishana Mawazo na Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo,Dr. Fennella Mukangara (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Dr. Elisante Ole Gabriel (kulia) leo mjini Mbeya mara baada ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa 2012.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennella Mukangara (kulia) pamoja na Naibu wake,Mh. Amos Makalla (katikati) wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera,wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa 2012,iliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Kikundi cha Simba Machezo cha Jijini Mbeya kikitumbuiza jana wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2012.Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO-MBEYA.
0 Comments