Jopo la wataalamu wa masuala ya afya nchini Marekani kwa mara ya kwanza limeafiki na kuunga mkono dawa ambayo inaweza kutumika kama kinga dhidi ya virusi vinavyoeneza ukimwi.

Jopo hilo limependekeza kwa Mamlaka inayosimamia chakula na Dawa nchini Marekani dawa wakubali dawa aina ya Truvada,itumiwe na watu ambao wamo hatarini kukumbwa na virusi vinavyosambaza ukimwi.



Hata hivyo Jopo hilo halina mamlaka juu ya wakuu hao ingawa mara nyingi hukubaliana.

Wahudumu kadhaa wa Afya pamoja na makundi yanayoshughulikia tatizo la ukimwi wamepinga dawa hio isiruhusiwe.

Hata hivyo, wandishi wanasema kua hatua hio inaweza kutokea kua muhimu katika vita dhidi ya ukimwi.

Tayari dawa ya Truvada imeisha idhinishwa na mamlaka hio ya dawa na chakula kwa watu wanaishi na virusi vya ukimwi, ikitumiwa sambamba na dawa zilizopo maarufu kama ''anti-retroviral drugs''.

Utafiti uliofanywa mnamo mwaka 2010 ulionyesha kua 'Truvada', iliyotengenezwa na kampuni yenye makao yake huko Carlifornia, Gilead Sciences, kwa kiwango ilipunguza hatari ya kuambukizwa ukimwi miongoni mwa wanaume wenye tabia ya kufanya mapenzi na wanaume wenzao kwa asili mia 44% na 73%.

Uwamuzi mwezi Juni

Kamati inayotoa ushauri kuhusu dawa zinazostahili kutumiwa kwa kukabiliana na ukimwi, FDA, ilipitisha kwa kura 19 kwa 3 kuafiki dawa hii itumiwe na watu ambao wamo katika hatari kubwa kuweza kuambukizwa - wanaume ambao wana tabia ya uzinzi na wanaume wenzao wengi.

Vilevile waliidhinisha dawa hii kwa kura nyingi, itumiwe na watu ambao hawajaambukizwa lakini wakiishi na wapenzi ambao tayari wanaishi na virusi vya ukimwi na halikadhalika kwa makundi yanayotazamiwa kua hatarini kuambukizwa ukimwi kupitia shughuli za ngono.

Upinzani kwa dawa hii ulitegemea dhana kua inaweza kutoa sura kwa mtumiaji kujihisi kua ana kinga mwilini, na hivyo kutoka ovyo, na pili hofu ya dawa hii ni uwezekano wa kuzua balaa la ukimwi mpya usiokubali dawa au tiba.


Vilevile kuna wasiwasi kua bei kali ya Truvada inaweza kuathiri kiwango cha fedha za shughuli nyingine za kutafuta dawa yenye bei nafuu kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Muuguzi mmoja Karen Haughey aliliambia Jopo kua : "dawa hii 'truvada' lazima itumiwe kila siku, wakati wote, siku hadi siku, asili mia 100% ya mda wako, na kwa uzowefu wangu naona kama hilo halitowezekana.

Hata hivyo wauguzi wengi walifurahia pendekezo la Jopo.

Mkurugenzi mtendaji wa juhudi za kinga ya virusi vya ukimwi, Mitchell Warren alisema baada ya kura hio kua "hili linatufikisha ukingoni mwa kufanikiwa katika kupata kinga dhidi ya ukimwi.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) inatarajiwa kufikia uwamuzi wake kabla ya tareh 15 Juni.V