Mmoja wa majeruhi akilia kwa maumivu.
Mmoja wa majeruhi akipewa msaada wa kupepewa na wasamaria wema baada ya kuzirai.
Mmoja wa majeruhi akipewa msaada wa kupepewa na wasamaria wema baada ya kuzirai.
Askari wa kikosi cha uokoaji cha Ultimate Security wakitoa msaada.
Dereva wa Gari aina ya Alteza Zuhura Nyamatama (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa askari wa usalama Barabarani jinsi ajali hiyo ilivyotokea.
Pichani juu gari ikiondolewa eneo la tukio.
Na.MO BLOG
Abiria kadhaa wamenusurika kufa baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria ‘daladala’ aina ‘coaster’ na gari dogo aina ya Toyota ALTEZZA.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi majira ya saa 2:40 katika eneo la barabara ya Kaunda karibu njia panda ya kwenda Masaki.
Kwa mujibu wa Jofrey Mwakibete wa Mo Blog aliyekuwa mmoja wa abiria katika daladala hizo, daladala yenye nambari T 786 BWS iliyumba na kuigonga gari ndogo yenye nambari T 203 BXH iliyokuwa ikiendeshwa na Bi. Zuhura Nyamatama, na kisha kuigonga daladala nyingine iliyokuwa mbele yake.
Baada ya kusababisha ajali hiyo dereva na kondakta wa gari walikimbia.
Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ila abiria kadhaa wamejeruhiwa kutoka na ajali, wengine kutokana na kukanyagana waking’ang’ania kutoka nje huku wengine wakipata mshituko.
0 Comments