Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO , Yusuph Al Amin akionyesha jinsi gani radio ya solar inavyofanya kazi mara baada ya kukabidhi Radio 200 kwa wakazi wa kijiji cha Ololoskwan wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa Radio jamii ulioanzishwa chini ya udhamini wa Airtel kwa kushirikiana na UNESCO. Ololosokwan Radio inategemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Juni, wanaoshuhudia kushoto ni mwakilishi wa Airtel Ahmed Juma katikati ni Yannick Ndoinyo Mkurugenzi Mtendaji IrkiRamat Foundation (RAMAT).
Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO, Yusuph Al Amin akikabidhi radio ya solar kwa mkazi wa kijiji cha Ololosokwan wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa Radio jamii ulioanzishwa chini ya udhamini wa Airtel kwa kushirikiana na UNESCO. Radio zaidi ya 200 zilikabidhiwa kwa wakazi wa kijijini hapo, uzinduzi wa radio hii utafanyika mwishoni mwa mwezi Juni.
Wanakijiji wa Ololoskwan na wawakilishi wa UNESCO na Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembela mradi wa radio unotegemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Juni.
Wafanyakazi wa Airtel, Dua Kazimoto na Mercy Nyange wakiwa katika picha na wanawake wafanyabiashara wa vikundi vidogovidongo wa kijiji cha Ololosokwan wakati walipotembela mradi wa radio unaotegemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Juni.
0 Comments