Kikosi cha timu ya taifa cha Italy ambacho kimefanikiwa kuingia nusu fainali za euro 2012 baada ya kuifunga kwa penati timu ya taifa ya Uingereza.
Kikosi cha timu ya taifa ya England ambacho kimetolewa mashindanoni na Italy baada ya kushindwa katika mchakato wa penati.
Penati ya ushindi kwa timu ya Italy iliyopigwa kiufundi zaidi na mchezaji Diamant na kuipeleka timu ya taifa ya Italy kwenye nusu fainali za euro 2012.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya Italy wakitimua mbio za ushindi baada ya mchezaji Diamanti kufunga goli la ushindi kwa njia ya penati dhidi ya timu ya taifa ya Uingereza.Timu ya Italy imefanikiwa kuingia nusu fainali za euro 2012 kwa kuifunga timu ya taifa ya England kwa jumla ya goli 4-2 baada ya kutoka 0-0 kwa dakika 120.