Jengo la Utawala la Sekondari ya kumbukumbu ya Sokoine inayojengwa Wami Ruhindo, Wilayani Mvomero.
Meneja uzalishaji wa Kiwanda cha Nguo cha Mjini Mvomelo, Clement Munisi (aliyenyosha mkono) akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotembelea kuona athari za maji machafu yenye kemikali za sumu yanayohifadhiwa katika mabwawa ya maji ambayo yanatiririsha maji hadi ndani ya mto Ngerengere na kusababisha madhara makubwa ya afya za binadamu na viumbe hivyo ikiwemo mimea na mifugo
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Morogoro , watendaji wa kiwanda cha Ngozi kilichopo eneo la Kihonda wakiangalia sehemu ya kukusanya maji machafu yenye kemikali za sumu kabla ya kuingia kwenye mabwawa maalumu.
Moja ya mabwawa ya maji machafu yenye kemikali zenye sumu yaliyohifadhiwa baada ya kuwekwa dawa ya kusafisha sumu hizo , sehemu ya maji hayo hutiririka kwenda kuingia kwenye mto Ngerengere na kusababisha madhara ya afya za binadamu pamoja na viumbe vingine ikiwemo mifugo na mimea.Picha na John Nditi.
0 Comments