Mtu mmoja amefariki na wengine 15 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha msafara wa rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Gari mojawapo katika msafara huo liligongana na gari la abiria karibu na mji wa Zvimba, ikiwa ni ajali ya tatu katika kipindi cha wiki mbili.
Msemaji wa Polisi Wayne Bvudzijena amesema ajali hiyo imetokea kutokana na basi hilo kushindwa kupisha msafara huo kwa haraka.
Kwa kawaida rais Mugabe husafiri na msafara wa magari takriban 10.
Msafara wake unahusisha gari la kifahari la rais, pikipiki na magari ya jeshi.