Iran imefutulia mbali ziara ya afisa wake mmoja mkuu wa wizara ya mambo aliyetarajiwa kusafiri nchini Saudi Arabia.
Hii inafuatia mzozo kati ya nchi hizo mbili kuhusu kunyongwa kwa raia wawili wa Iran waliokamatwa nchini humo kwa makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
Shirika la habari la Mehr nchini Iran limesema kuwa afisa huyo alitarajiwa kumwalika waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Saud al-Faisal, kwa mkutano maalum nchini Iran.
Tehran imewasilisha malalamiko kuhusu hukumu hiyo ya kunyongwa kwa raia hao.
Inasema kuwa walizuiliwa kwa miaka mitano na kutoruhisiwa kuwasiliana na maafisa wa ubalozi pamoja na mawakili au hata wakalimani.