Waandamanaji mjini Khartoum, Sudan, wametumia matairi waliyoyaasha moto na mawe kuwazuwia polisi waliojaribu kuzima maandamano dhidi ya serikali kupinga hatua ya serikali ya kubana matumizi.
Maandamano hayo awali yaliongozwa na wanafunzi, lakini inaarifiwa na wananchi wengine nao wamejiunga nayo.

Polisi wa Sudan wameamrishwa kuchukua hatua haraka kumaliza fujo hizo.

Maandamano hayo yaliyoanza tarehe 16 Juni, yalichochewa na hatua za serikali za kupambana na msukosuko wa kiuchumi, uliotokana na Sudan Kusini kusimamisha kusafirisha mafuta yake kwa kupitia Sudan.