Omar Sulaiman

Omar Suleiman, mtu aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi nchini Misri chini ya utawala wa rais aliyeondolewa mamlakani Hosni Mubarak, amefariki akiwa nchini Marekani.
Generali Suleiman alifariki hospitalini mapema leo kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la Mena.
Msaidizi wa generali huyo alisema kuwa kifo chake kimetokea ghafla wakati alipokuwa anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Hayati Suleiman aliteuliwa kama makamu wa rais kuhudumu katika siku za mwisho za utawala wa Mubarak.
Hata hivyo alikuwa na nia ya kugombea urais mwaka huu lakini akaondolewa nje ya shughuli hiyo kwa sababu zisizojulikana.
"alikuwa sawa tu. Lakini ghafla ikatokea tu alipokuwa anapokea matibabu mjini Cleveland," alisema msaidizi wake, Hussein Kamal.
Bwana Kamal alisema kuwa maandalizi yanafanywa ili kuleta mwili wake nchini Msiri kwa maziko.