Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, UNBOA wakiwa katika picha ya pamoja na Msimamizi Mkuu wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bi Susan Malcora mara baada ya ya Tanzania na Afrika ya Kusini kuachiana kijiti. Tanzania ilipitishwa kwa kauli moja na Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, kuwa mjumbe wa Bodi ya UNBOA ambapo itafanya kazi na wajumbe wengine wawili ambao ni China na Uingereza.

Naibu Mkaguzi Mkuu kutoka Afrika ya Kusini Bw. Thembele Makwetu akimkabidhi mkoba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh,ikiwa ni ishara rasmi ya Ofisi yake kuingia katika Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa. Mdhibiti na Mkaguzi na Ofisi yake anachukua nafasi inayoachwa wazi na Afrika ya Kusini ambayo imekuwa mjumbe wa Bodi hiyo kwa miaka 12. Tanzania kupitia Ofisi ya Mdhibiti Mkuu itashika nafasi hiyo kwa miaka sita. Wanaopiga makofi kutoka kushoto ni Mkaguzi Mkuu kutoka Uingereza Bw. Amyas Morse ambaye naye ni mjumbe wa Bodi na Bw. Dong Dasheng jumbe wa Bodi pia na ni Naibu Mkaguzi Mkuu kutoka China.