KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine
inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwa ajili ya abiria waendao Dar es
Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed
Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.
Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli
hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo
abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam
ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na
Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha
kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa
ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda
kasi ya notkomail 20

0 Comments