Mchezaji wa timu ya Simba ya Tanzania Felix Sunzu akimiliki mpira mbele ya Ilongo Ilifo beki wa timu ya Vital Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa kombe la Kagame uliofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo timu hizo zimetoka sare ya magoli 1-1
Kikosi cha timu ya Vital Club kutoka DR Congo kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo.

Kikosi cha timu ya Simba ya Tanzania kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo

Mashabiki wa timu ya Simba ya Tanzania wakiwa wamesimama dakika moja kukumbuka waliokufa katika ajali ya boti baharini huko Zanzibar.