Viongozi wa Afrika Magharibi wanakutana Burkina Faso kuzungumzia msukosuko wa
Mali.
Jumuia ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS inafikiria kuingilia kati kijeshi,
baada ya kundi la Kiislamu na wapiganaji wa kabila la Tuareg kuliteka eneo la
kaskazini, kwa kutumia fursa ya udhaifu wa serikali kuu wakati wa mapinduzi ya
Mali.
Rais Blaise Campaore wa Burkina Faso, alisema lengo la mkutano ni kujadili
kile alichoelezea kuwa tishio la kigaidi kaskazini mwa Mali, na kutafuta
ufumbuzi katika msukosuko wa siasa nchini Mali.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bado halijakubali kuingilia kati
kijeshi nchini Mali.
|
0 Comments