Hii ni moja ya wodi ya kina mama wanaojifungua (wodi ya wazazi),kiukweli hali hii mimi binafsi inanisikitisha sana kila nikikaa chini kufikiria idara husika.Kwa kweli kama mmoja wa kiongozi nchini atafanikiwa kutembelea wodi za wazazi nchini sidhani kama usiku atalala usingizi.


Viongozi wetu tuliowachagua kwa ridhaa zetu na kuwaamini kwa Imani kuwa mtatuletea mabadiliko nchini kwenye sector mbalimbali tafadhalini kama hamuoni au kusikia haya,basi nawawekea na picha kabisa muone kina mama wanavyoteseka mahospitalini.


Nimeweka picha hii sio kama nachochea kitu laahasha na msinihukumu waungwana,hii ni kukumbushana mambo baadhi ya sehemu hayaendi sawa.