Habari nilizozipokea kila kona ya dunia leo hii kuhusiana na kuzama kwa Meli kisiwani Zanzibar.Nachukua nafasi hii kutoa pole zangu kwa wahusika wote waliopatwa na ajali hii kwa namna moja ama nyingine.

Msiba huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu na ikizingatiwa si kipindi kirefu tokea maafa yaliyotokea miezi michache iliyopita ajali kama hii.Maganga One Blog na team nzima inatoa salamu za rambirambi kwa ndugu,jamaa na marafiki kwa waathirika wote wa ajali hii.Tuwe katika kipindi cha subira kwani hali hii ni nzito kwa kila mmoja wetu.

Nawaombea kwa Allah s.w wale wote waliotangulia mbele ya haki kutokana na ajali hii wakalale mahala pema peponi.Tutawaletea picha za matukio ya ajali kwa kadri tutakapozipata.Pole tena na tena kwa waathirika wote wa ajali hii.
                                          Maganga One Blogger.