Rais wa kwanza wa kiraia wa Misri, na kutoka chama cha Kiislamu, Mohammed Morsi,
ameapishwa, na ametoa wito kuwa bunge la nchi lirejeshwe haraka - bunge
lilofutwa hivi karibuni.
Katika sherehe kwenye eneo la jeshi nje ya Cairo, kiongozi wa wakuu wa jeshi
wanaoongoza nchi, Field Marshal Mohammed Tantawi, alikabidhi madaraka rasmi kwa
Rais Morsi.
Hapo awali, akitoa hotuba yake ya kwanza iliyogusia mambo mengi, katika Chuo
Kikuu cha Cairo, Bwana Morsi alisema atalilinda jeshi kama taasisi, lakini piya
alionya jeshi halifai kuwa mbadala wa matakwa ya wananchi.
Bwana Morsi aliahidi ukurasa mpya utaong'ara katika historia ya nchi,
kufwatilia ule aliosema ni ukurasa wa kuchusha.
Alipokuwa akizungumza, akina mama ambao watoto wao waliuliwa chini ya utawala
wa Rais Mubarak, walibeba juu picha za watoto wao hao wa kiume.
Bwana Morsi piya alisema Misri haitotapakaza mapinduzi nchi za nje.
Rais mpya aliapishwa kwenye sherehe iliyofanywa katika mahakama ya katiba
mjini Cairo. |
0 Comments