Mwendesha mashtaka mkuu nchini Misri, ameaumuru rais wa zamani wa nchi hiyo,
Hosni Mubarak kurejeshwa gerezani akisema kuwa hali yake ya afya imeimarika
sasa.
Mubarak, mwenye umri wa miaka ,84, alihamishwa kutoka gerezani humo mwezi
jana baada ya ripoti za afya yake kuzorota .
Alisemekana wakati huo kuwa alipatwa na kiharusi mwa mpigo na kuwekwa kwenye
mashine ya kupiga moyo. Ripoti za Mubaraka kupoteza fahamu wakati huo zilipingwa
vikali.
Mwezi Juni , Mubarak alihukumiwa kifungo jela baada ya kupatikana na hatia ya
mauaji ya waandamanaji waliokuwa waanpinga utawala wake.
Mkuu huyo wa mashtaka, Abdel Maguid Mahmoud alitoa agizo la kumhamisha rais
Mubaraka kutoka hospitali ya kijeshi ya Maadi hadi katika hospitali ya Tora
baada ya afya yake kuimarika.
Naibu wa Mahmoud, Adel al-Saeed, ilisema kuwa jopo la madaktari lilikuwa hapo
awali limesema kuwa afya ya rais huyo wa zamani iko sawa sasa mradi atumie
madawa yake na kwamba kwa mtu mwenye umri wake hilo ni sawa.
Hata hivyo haikujulikana mara moja lini Mubaraka atarejeshwa tena
gerezani.
Aidha mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa taarifa zozote kuhusu afya
yake, wamisri wanazichukua kwa shauku kubwa.
Kumekuwa na shauku kubwa kuhusu afya ya Mubarak wengi wakisema kuwa taarifa
zozote kuhusu afya ya Mubarak zinatafsiriwa kama njama ya yeye kutaka kutolewa
gerezani kwa misingi ya afya yake.
Hata hivyo wengi wanajua kuwa huu sio mwisho wa wao kusikia kuhusu sakata hii
ya afya ya Mubarak.

0 Comments