Mji Mkuu wa Uchina, Beijing, umepata mvua kubwa kabisa kuwahi kutokea kwa zaidi
ya miaka 60.
Watu kama 10 wamekufa, na maelfu wamehamishwa makwao.
Mvua kubwa ya jana ilifurika mabara-barani, kupeperusha mapaa, na kuporomosha
miti na milingoti ya taa.
Maji mjini yalikuwa yanafika kiunoni.
Safari za ndege zaidi ya mia mbili zilivunjwa, na hivo kuwaacha maelfu ya
watu wamenasa kwenye viwanja vya ndege.
Mvua sasa imeanuka mjini Beijing, lakini mvua kubwa inatarajiwa
kaskazini-mashariki na kusini-magharibi mwa Uchina.

0 Comments