Kama kawaida toka enzi hizoo,ikifika wakati wa likizo nakumbuka wazazi wangu walikuwa wakipenda kutupeleka kwa babu na bibi zetu mikoani,na ukifikia umri fulani wa ukubwa yale mazoea uliyozoeshwa na wazazi kwamba kila likizo lazima urudi kijijini kwenu uendelea mpaka ukubwani.Kwa upande wangu upendelea kujifunza mengi kutokana na likizo kwa kusafiri mkoa mpaka mkoa mwingine.Pichani nikiwa nimepozi na kukumbuka enzi hizo tunamsubiri dereva ndio tuanze safari.
Nakumbuka wazee wangu walipendelea msemo usemao ``Abiria chunga mzigo wako`` na hapo kila nikiukumbuka ule msemo ujikuta mzigo wangu siubandui mkononi kama picha inavyojidhihirisha.
Wapenzi wangu na wasomaji wa Maganga One Blog napenda kuchukua fulsa nyingine tena kuwaomba radhi sana kutokana na mambo mawili muhimu yanayoendelea hivi sasa na kusababisha kutowaridhisha wasomaji wangu.
1.Matengenezo ya Blog yanayoendelea hivi sasa ili kuleta muonekanao mzuri wa Blog yenu.
2.Likizo niliyopo hivi sasa na safari za mikoani kama mnionavyo pichani zinasababisha kuchelewa kuwatelea habari kwa muda muafaka.
Nawaomba radhi sana kwani mambo yapo nje ya uwezo wangu na nitajitahidi baada ya wiki mbili kuyarejesha kama awali.
Ni matumaini yangu kwamba kila mmoja ananielewa vyema na kukubalina na mimi.Nawaahidi kurejea jukwaani kama kawaida kila nikipata chance ya kufanya hivyo.nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu na kuwa bega kwa bega na blog yenu ya Maganga One.
Maganga One.
0 Comments