Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kisaka saka na Baadhi ya makamanda wa Kikosi
cha 672 cha JWTZ kiliopo Kisaka saka kufuatia tatizo lililojitokeza ya umiliki
wa Ardhi kati ya pande hizo mbili. Kushoto ni ya Balozi Seif ni Mkuu wa Kambi
hiyo Kanali Omar Suleiman Mateka na Kushoto ya balozi Ni Mkuu wa Wilaya ya
Magharibi Nd. Hassan Mussa Takrima
Baadhi ya Makamanda waliokuwa wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ya kuunda Kamati ya kutafuta muafaka wa Umiliki wa Ardhi kati ya JWTZ na Wananchi wa eneo la Kisaka saka.
Kundi la Wananchi wa Kisaka saka wakimsikiliza
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia tatizo la Ardhi
lililojichomoza baina ya Wananchi wa eneo hilo la Kambi ya JWTZ iliyopo Kijijini
hapo.
Na Othman Khamis Ame
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi ameelezea umuhimu wa kuondoshwa sintafahamu iliyopo baina ya Wananchi
wa eneo la Kisaka saka na Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ } iliyopo
katika eneo hilo ili kuendeleza ujirani mwema kati ya pande hizo mbili. Balozi Seif alieleza hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Eneo la Maungani, Kombeni na Fuoni pamoja na Uongozi wa Jeshi hilo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi hao pamoja na Taarifa ya Jeshi hilo kufuatia tatizo la mipaka ya Ardhi lililojichomoza baina ya pande hizo mbili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
alisema hakuna haja ya uhasama kati ya Askari na Raia na kusisitiza kwamba pande
hizo mbili ni vyema zikaendelea kuheshimiana.
Balozi Seif aliagiza kuundwa mara moja kwa Kamati ya Pamoja Kati ya Uongozi wa Jeshi hilo na Wananchi hao kwa kushirikisha pia na Watendaji wa Taasisi zinazosimamia Suala la Ardhi chini ya Mkuu wa Wilaya ya Magharibi.
“ Hii Kamati naipa muda wa mwezi mmoja na Mkuu wa Wilaya ahakikishe ananiletea jibu la hatma muwafaka la tatizo hili ifipako mwishoni mwa Mwezi wa Agosti” Alisisitiza Balozi Seif.
Alifahamisha kwamba hakuna sababu ya kuendeleza mtafaruku baina ya Jamii na Taasisi za Serikali na kushauri hekima itumike zaidi wakati yanapojitokeza matatizo hasa ya ardhi.
Balozi Seif alisema Taratibu za Askari kutumia
ubabe wakati Wananchi watapandisha jazba katika kutafuta haki ya umiliki wa
Ardhi kunaweza kuleta athari ya kudumu hapo baadaye.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliendelea
kuikumbusha Jamii kwamba Ardhi itaendelea kuwa Mali ya Serikali jambo ambalo
linaelezwa kila wakati. Balozi Seif alifafanua kwamba Serikali wakati wote
huamua kulipa fidia ya Majengo au Vipando kwa Wananchi watakaoathirika kutokana
na Maamuzi yake ya kuitumia Ardhi hiyo kwa shughuli za Taasisi zake
zinazohudumia Wana Jamii wote.
Alisema katika kukabiliana na tatizo la Ardhi
Serikali imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo kwa watendaji wake,Viongozi na hata
Masheha ili kulielewa vyema suala hili linaloonekana kuleta migogoro kila
kukicha. “
Mimi na wasi wasi na suala hili la migogoro ya
Ardhi kwamba baadhi ya Viongozi walio wengi wanaliogopa kwa kuhofidha lawama
miongoni mwa wanaowaongoza kwa sababu semina tunatoa lakini utekelezaji wake ni
hafifu”. Alifafanua Balozi Seif. Mapema wakitoa malalamiko yao baadhi ya Wananchi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya walalamikaji wa eneo hilo la Ardhi walielezea masikitiko yao kutokana na Jeshi hilo kutanua eneo la Mipaka ya Ardhi bila ya kushirikishwa wao katika awamu ya Pili sasa.
Wananchi hao waliomba kuwepo na mipaka ya
kudumu ya eneo la Jeshi hilo itayokubalika na pande zote mbili kwa lengo la
kuepuka migogoro inayoweza kudhibitiwa mapema.
Akitoa Taarifa ya Kikosi cha 672 Mkuu wa Kambi
hiyo iliyopo Kisaka saka Canal Omar Suleiman Mateka alisema kwamba ramani ya
sehemu hiyo inaonyesha kuwa eneo hilo lilikuwa la malisho ya Mifugo wakati kambi
hiyo inaanzishwa rasmi Mwaka 1978.
Canal Omar alieleza kuwa matatizo ya ardhi
baina ya Jeshi na Wananchi walioizunguuka Kambi hiyo yamejichomoza Mwaka 2008 na
kupelekea Mkuu wa Brigedia Nyuki kuagiza kufanywa kwa Vikao kwa pande husika
katika miaka ya 20011 kufuatia Barua za Malalamiko kutoka Kwa Wananchi
hao.
Mkutano huo ulihusisha pia Naibu waziri wa
Ardhi,Maendeleo ya Makaazi, Nishati na Madini Zanzibar, Watendaji wake pamoja na
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi.
1 Comments
and found that it's really informative. I'm going to watch out for brussels. I'll be grateful if you continue this in future. Numerous people will probably be benefited out of your writing. Cheers!
Also visit my website : Secure Your Cure