Abiria wa wakishushwa kupitia madirishani baada ya Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na Basi la Simba mtoto lililokuwa linaenda Tanga kugongana uso kwa uso maeneo ya Wami kiasi cha masaa mawili hivi yaliyopita. Mwanahabari wa Globu ya Jamii aliyekuwa eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna maafa yaliyoropotiwa ila watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado hakijafahamika.
Uso kwa uso

                 Abiria wakijaribu bila mafanikio kumuokoa mwenzao aliyenaswa
                                                       Mmoja wa majeruhi
                        Mama akiwa anaugulia pembeni mwa barabara
Abiria wakiendelea na juhudi za kuwatoa wenzao kutoka katika mabasi hayo