BONDIA
Rashid ‘Snake Man’ Matumla juzi alipigwa kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya
nne na Benjamin Simon wa Ujerumani, katika pambano lililokuwa la raundi 12, la
kuwania taji la IBF, uzito wa Super Middle lililofanyika kwenye ukumbi wa
Universal, Berlin, Ujerumani. Hilo lilikuwa pambano la pili kuwakutanisha
mabondia hao, awali Matumla alishindwa kwa pointi, ila juzi ‘alipotea mapema’.
Matumla alitafutiwa mechi hiyo na bondia maarufu wa zamani nchini, Ally Bakari
‘Champion’ kwa kushirikiana na African Camp Promotion ya Nairobi, Kenya, chini
ya Mkurugenzi wake, Thomas Mutua. Matumla anarejea nchini leo. Pichani ni refa
Jean Pierre akimuinua juu mkono Benjamin kumtangaza mshindi dhidi ya Matumla
kushoto.

0 Comments