Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kwamba katika makao makuu wa jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia kuna washauri 10 wa kijeshi toka Uingereza.
Jeshi hilo la Umoja wa Afrika limekuwa ndani ya Somalia likipambana na wapiganaji wa Al shabaab ambao wanadhibiti maeneo mengi nchini Somaia
lakini mwandishi wa BBC amesema kuwa baadhi ya maafisa hao wanaosemekana kuwa ni washauri wameonekana maeneo ya Afgoye ambao hivi majuzi ulutekwa kutoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab.
Kundi la al-Shabab ambalo mapema mwaka huu lilijiunga na al-Qaeda linadhibiti maeneo mengi nchi Somalia.mengi ya maeneo hayo yako Kusini na katikati mwa Somalia.
Hata hivyo Al shabaab kwa wakati huu wamebanwa kutoka pande zote.
0 Comments