Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amesema amefadhaishwa na ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo imesema maafisa wa Rwanda wanawasaidia waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katibu Mkuu huyo amefanya mawasiliano na na Rais Paul Kagame wa Rwanda pamoja na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuzungumzia ghasia ambazo zimezuka tena katika mkoa wa Kivu Kaskazini baada ya kundi la askari kuasi jeshi.