Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Ummy Mwalimu akicheza ‘kwaito” na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kibaigwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa mabweni 30 nchi nzima kwa mtoto wa kike.
Waziri kivuli wa Elimu na mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Susan Lyimo akiongea katika hafla ya uchangiaji wa mabweni. Katika hafla hiyo jumla ya shilingi 37,214,000/= zilipatikana ikiwa ni ahadi pamoja na fedha taslim.
Mgeni Rasmi, Waziri kivuli wa Elimu na mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Susan Lyimo akipokea mkasi kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya TEA Dkt Naomi Katunzi kwa ajili ya kuzindua rasmi harambee ya ujenzi wa mabweni 30 kwa ajili ya watoto wa kike wa sekondari nchini.
Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Kibaigwa Mhe. Job Ndugai Akivuta utepe uliokatwa na mgeni rasmi Mh. Suzan Lyimo huku tukio hilo likishangiliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na TEA.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa mchango wake na akihimiza watu wengine wachangie katika ujenzi huo. Ili mradi huo ukamilike jumla ya shilingi za kitanzania shilingi bilioni 2.3 zinahitajika.