Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza kucheza jana.
            Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mpambano huo.
Beki mpya wa Yanga aliyetokea Simba hivi karibuni, Kelvin Yondani, akimzunguka Torachi Brain.

Mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga ya Dar es Salaam jana iliichapa timu ya The Express ya Uganda mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hiyo ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu ya nchini humo. Katika mechi hiyo Yanga ilichezesha wachezaji wake wapya.