Na Gladness Mushi ~Arusha
Imebainika kuwa zaidi ya watu milioni 4 dunia kote
wanakufa kwa maradhi yasabaishiwayo na ugonjwa wa Kisukari huku watu wapatao
milioni 360 wanaugua ugojwa wa kisukari Dunia kote hii ni kwa mujibu wa takwimu
ya wanasayansi ya mwaka 2011.
Hayo yamebainishwa hii leo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bwana John
Mogela wakati akifungua rasmi
upimaji wa Kisukari kwa wakazi wa jiji la Arusha iliyoandaliwa na Hospitali ya
AICC kwa kushirikiana na Madokta wa kisukari kutoka mkoani Kilimanjaro sambamba
na wataalamu wa kimataifa.
Amsema kuwa upimaji huo ni muhimu sana kwa wakazi wa jiji
la Arusha kwa maana wataweza kujitambua
hali za afya zao wakazi wa jiji la Arusha
kwa maana huduma za upimaji wa Kiusukari na utibuji wake ni gharama
kubwa sana.
Aidha amewataka wakazi wa jiji la Arusha kubadilisha mfumo
wa maisha kwa kufanya mazoezi kuacha uvutaji wa sigara pamoja na unywaji pombe
ambapo ni vitu vinavyochangia kwa kiasi kiukubwa maradhi ya kisukari.
Kwa upande wake mkurugenzi wa AICC bwana Kaaya amesema kuwa upimaji
huo umeletwa kutokana na hao AICC
kuona kuwa kulikuwa na mkutana wa wataalamu wa Kisukari hapa jijini na kuona
hiyo ndio fursa nzuri ya kuwatumia wataalamu hao katika utoaji huo
wa bure upimaji huo
|
0 Comments