Assalam Aleykum.
Nawatakia Eid Mubarak kwa waislamu wote duniani...Maganga One Blogger nawapongeza waislamu wote kwa kufunga salama mfungo mtukufu wa Ramadhani na leo iwe siku nzuri kwa kusheherekea siku hii kwa amani.

Tule na kufurahi kwa pamoja.
                                            TANGAZO
Kwa wailaslamu wote na wale watakaopenda kujumuika pamoja katika kula na kusherehekea pamoja sikukuu hii ya Eid el Fitr nchini Ubelgiji,Umoja wa nchi za Afrika tunaozungumza lugha ya kiswahili tumeandaa chakula cha pamoja ili tujumuike kusheherekea siku hii tukufu kwa pamoja.Hivyo kwa kila atakaejisikia kuja Ruksa.

Jinsi ya kufika mahala hapo anuani ni kama ifuatavyo.
(Praatpunt~Geel)
Logen 104
2440 Geel.

Kwa wale watakaotoka Antwerpen wapande bus no 416 au 417 wakifika Turnhout wapande bus no 490 au 492 kuelekea Westerloo au St Dimpna Hospital na kituo cha kushuka ni St Dimpna hospital,wakifika hapo ni kuuliza wapi  Geel Praatpunt no 104.

Kwa watakaotumia usafiri binafsi kwenye tomtom zao wajaze adress hiyo hapo juu ambayo ni Logen 104,post code no 2440 Geel.

Tunategemea kushirikiana pamoja katika sikukuu hii tukufu siku ya leo.
                                     Ahsanteni sana.