Familia za wachimba migodi waliouliwa na polisi wa Afrika Kusini, wakati wa
mgomo wa Alhamisi, zimekuwa zikipita mahospitali kuwatafuta jamaa zao.
Wake wa wachimba migodi wanasema polisi na mameneja wa kampuni ya mgodi
hawakuwapa orodha ya wachimba migodi 34 waliouwawa na wengine wengi
waliojeruhiwa kwenye mapambano hayo.
Polisi wanasema sasa wanashirikiana na mameneja wa mgodi kutoa orodha kuu,
lakini haiwezi kufichua majina ya wachimba migodi zaidi ya 200 waliokamatwa.
Rais Jacob Zuma ametangaza kuwa ataunda tume ya kuchunguza mauaji hayo.
Rais wa chama cha wafanyakzi kisichokuwa rasmi, ameiambia BBC kwamba wanataka
tume ya kimataifa na iliyo huru.
Polisi wanasema watu thelathini na wanne waliuwawa katika tukio hilo.
Rais wa chama cha wafanyakazi ambacho siyo rasmi, Joseph Mathunjwa, wa
Association of Mineworkers and Construction Union, aliiambia BBC kuwa wanataka
tume huru ya kimataifa kuchunguza mauaji hayo kwa sababu chama chake tayari
kinalaumiwa kwa ghasia hizo.
Kampuni inayomiliki migodi hiyo, Lonmin, imeahidi kusaidia familia za
walioathirika, lakini inashikilia kuwa mgomo huo hauku
Watu kumi wakiwemo polisi wawili waliuwawa kabla ya tukio la siku ya Alhamisi.
wa halali.
Chama hicho kinataka nyongeza ya mshahara wa zaidi ya dola 1,000 kwa
mwezi.
0 Comments