Raia mmoja wa Somalia amehukumiwa vifungo 12 vya maisha na Mahakama ya Marekani baada ya kumuona kuwa na hatia ya kufanya makubaliano kwa niaba ya maharamia wa kisomali kuhusu fidia ya kuchiwa huru kwa mateka wa Marekani mwezi wa pili mwaka uliopita.
Raia huyo wa Somalia Mohammad Shibin (pichani) amekutwa na makosa 15 ya kiwemo ya uharamia na utekaji nyara.
Kwa mujibu wa mahakama hiyo Shibin alilipwa kati ya dola 30,000 na 50,000 kwa kufanya makubaliano ya fidia juu ya mateka hao.
Maharamia wa kisomali waliwateka raia wanne wa Marekani kwenye pwani ya Somalia na baadaye kuwauwa pamoja na jitihada za jeshi la Marekani kutaka majadiliano kuhusu kuachiwa kwao.
|
0 Comments